Labels

Tuesday, April 15, 2014

Papaa On Tuesday.....Heri Mvua Ikanyesha Ukajua Wapi Panavuja

Tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Siku ya leo na uzima aliotupa mimi na wewe tunapoelekea kuhitimisha majira haya ya Pasaka na tukiwa tayari kwa ajili ya kusheherekea kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Mbali na yote tunakila Sababu pia sisi kama Watanzania kumshukuru Mungu kwa ajili ya Kupatika kwa Hati ya Muungano ambayo kwa Miaka 50 imekuwa ikisadikika kuwa haipo kumbe ipo Ikulu kwenye makabati kabati nalo ni jambo la kumshuuru Mungu ni matumaini yangu kuwa sasa majadiliano kuhusiana na Muungano kule Bungeni yatafikia muafaka lakini isije kuwa kuwa kupatikana kwa hati ya Muungano ni Kuziba shimo la Panya kwa kipande cha Kitumbua tukiamini Panya wa Kero za Muungano hata tusumbua tena tatizo la Panya ataanza kula kitumbua pole pole tukija kustuka kumbe tulitumia tiba ya muda kwa gonjwa sugu.
Kwa siku kama 4 wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam na vitongoji vyake wamekuwa wakiishi kwa mashaka sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, kuna watu wamepoteza makazi, kuna watu wamepoteza ndugu, kuna barabara zimeharibika, kuna nyumba zimejaza maji, kuna madaraja yamekatika, kuna madaraja yamepata nyufa hii yote ni kazi ya Mvua. Kuna watu walihamia maeneo ambayo hawakujua nyakati za Mvua huwa kunafananaje wengine wamejenga maeneo hayo na kuna wengine wamepangishwa maeneo hayo yanaweza kuwa ya makazi ama biashara mwisho wa siku wamekuja pata picha halisi kuyafahamu mambo yaliyofichika. Kila jambo linalotokea na kulitazama inategemea sana na angle uliyokaa na kulitazama jambo hilo. Mfano inawezekana kabisa kukosa Bunge la Katiba watu kuongea kuhusu hati ya Muungano yamkini mpaka leo isingepatikana, pengine kupitia mvua zilizonyesha wangeni walisafiri kwa siri matokeo yake kubomoka kwa madaraja kukasababisha wajisalimishe kwa wapenzi wao kila jambo linalotokea basi kuna somo la kujifunza ndio maana ninasema ni heri Mvua ikanyesha Ukajua wapi panavuja.

Mgonjwa anapokuwa anaumwa na ukawa na kazi ya kuuguza kuna mambo ya kujifunza kuna wanaokuja kumuona mgonjwa, kuna wanamuuguza mgonjwa, kuna wanaokuja kumuonea huruma mgonjwa na kuna wanaokwenda kupata habari tu za mgonjwa na mambo mengi kama hayo. Jambo hili ni hata kwa wanaopatwa na mafuriko sio kila mtu anayekwenda anaenda toa msaada.Watu wanapokuwa wakija hospitalini ni wengi sana sana na wengine kuwa nani ni nani pia walikuwa wamefahamiana hapo, marafiki waliokuwa hajaonana muda mrefu walikutana hapo. Kuna waliokuja wakacheka, kuna waliokuja wakarudi na maswali mengiiii, kuna walikuja wakatoka na majibu ya maswali yao mengiii, kuna waliokuja na kuliaaa lakini mwisho wa siku nikasema kupitia kuugua  “Heri Mvua inyeshe tujue wapi panavuja”. Assume kama mgonjwa anayeumwa alikuwa na nyumba ya Siri mahali na alikuwa na mtoto pengine katika kulazwa kwake hospitali nyumba ndogo na mtoto nayo ikaja, watu ndo wakafunguka macho kweli kuumwa ni jambo baya lakini katika kuumwa kwake kuna jambo limefahamika.
Kama hakuna mvua nyumba za mabondeni na zenyewe zina raha yake full hewa, wale wa wanaokaa Jangwani huku Dar-es-Salaam wakati wa majira ya Kiangazi wana maisha mazuri kama wengine. Kwa wakazi wa maeneo korofi kama Sinza usiombe mvua ikanyesha ukajua maji yanavyojaa na kuziba barabara, kwa maeneo ya Kariakoo wakati wa mvua ndipo ambapo watu hufungulia chamber za maji taka. Ukitaka kuhamia kwenye nyumba mpya hamia wakati wa mvua ndipo utajua kuwa nyumba uliyohamia inavuja ama la. Kuna wakati ni heri mvua ikanyesha ukajua wapi pana vuja ili uweze kurekebisha.

Mvua inaponyesha na kugundua wapi panavuja kuna mambo matatu ya kufanya, kwanza kama tatizo lenyewe ni dogo unaweza kuziba kwa kumuita fundi ama ukaaamua kutengeneza mwenyewe sababu issue sio kubwa sana, jambo la pili ukigundua sehemu inavuja unataka kujua nini nimepelekea kuvuja kwa nyumba hapo sasa kunahitaji ukarabati wenye kugharimu kubomoa sehemu Fulani Fulani ili kuweza kuweka sawa pale panapovuja so hapo kuna gharama za fixing. Lakini njia ya tatu ni kuhama kabisa eneo hilo, kama kwa wakazi wa Jangwani ili kuepuka usumbufu wakati wa mvua ni kuhama maeneo yanayovuja sana na kuhamia maeneo salama.

Kuna watu ambao kwenye mahusiano yao ama ndoa zao kuna matatizo yanayohitaji tu marekebisho machache ili kuzuia tatizo lililopo, kuna watu wao wanahitaji aje fundi kabisa ndio wale unaowaona wanakwenda kwa washauri ama wazazi ama wasimamizi wa harusi zao nia na makusudi ni kusaidia kuzuia ndoa ama mahusiano kuharibika na kuna wale sasa ambao wao unaona wanaamua kabisa kuvunja ndoa zao na wengine kuachana nao kwa sababu gani uimara wa nyumba unapimwa wakati wa dhoruba.

Kwenye maisha kuna watu na taasisi zao inawezekana tukawa tunasema afadhari hili limetokea tumeujua ukweli, kuna mambo huwa yanatokea kama ajali, “coincidence” kwenye maisha kweli jambo linaweza kuwa ni baya lakini kupitia jambo hilo kuna ukweli mwingine uliokuwa umejificha huwa unajulikana. Unaweza kuta mtu ana watoto wa Siri amezaa na mtu mwingine kwenye Familia yake ya ndoa hawajui, siku akifa ndo wale watoto wanajulikana wakija mlilia mama ama baba yao. Unaweza kuta mdada kumbe alipataga mtoto zamani akaenda mficha kwa “bibi yake” huko kijijini na huku mjini mdada akaendelea na maisha yake, siku ikitokea Yule mtoto kule kijijini akaumwa ama akafa basi kuna jambo lingine huwalinatokea kwa kujulikana ni kama “Coincidence” Fulani ndo maana unasikia mtu “heri nimeujua ukweli”.

Katika mambo mengi sana yanayotokea kwenye maisha yetu kuna upande wa hasara na kuna upande wa kujifunza kile ambacho kinatokea. Pamoja na ubaya wa jambo kuna heri ya jambo hilo ndio maana katika msiba kuna Kufa Kufaana, lakini kuna mambo ambayo yanapelekea jambo lingine kufahamika kwa sababu ya tatizo lililotokea. Mvua ikinyesha tunajua wapi panavuja kama isingenyesha yamkini tusingefahamu lolote. Hujawai ona mwanaume kila siku simu yake iko mkononi siku hiyo ikatokea pengine ugonjwa ama kusahau simu nyumbani ndipo mkewe akaamua kuichukua simu hiyo na kukagua Hamad, anakutana na vitu vya ajabu, pengine ndipo anapogundua mume wake ni Shoga ama anauza madawa ya kulevya yapo mambo mengi sana yanayoonekana kama ni tatizo lakini kuna somo la kujifunza.
Kwenye maisha ya biashara unaweza kuta kila siku unapata hasara, kwa kupata hasara unaweza kujua hasara inatokana na nini. Hasara inakupa sababu ya kuboresha biashara yako. Heri ukapata hasara ukajua safari ya pili nini kilipelekea hasara mara ya kwanza. Ukijua wapi panavuja itakupa fursa ya kujiimarisha upya.

Kwenye mahusiano kuna watu wengi sana wanachukuaga maamuzi yasiyo sahihi kwa kugundua mtu wake kumbe anatabia Fulani. Wengi hutafuta suluhu ya kuhama badala ya kuangalia kama sehemu yenye tatizo inaweza rekebishika, ama inahitaji kubomolewa kwa maana ya kutoa maelekezo na njia mbadala badala ya kukimbilia kumuacha mtu. Assume mtu unayempenda kwa dhati ukagundua kumbe ana mtoto wan je ya ndoa, then wewe uka opt kuondoka na kumuacha utakuwa umejenga ama umebomoa? au unamuacha mtu sababu anatafuna vibaya ama akilala anakoroma na wewe hupendi wa kukoroma, heri umejua anakoroma ili uweze msaidia. Kuna wanawake hawapendi wanaume waongea kwa hasira, au wenye hasira wanatamani wanaume ambao ni reasonable hawawezi fanya kituko mbele za watu yaani hawawezi waabisha, kama watu hao hawajaoana mshukuru Mungu kuwa Heri Mvua imenyesha ukajua wapi panavuja, Kama Mtu wako sio mwaminifu na umegundua cha msingi usianze mtukana jiulize tu hii mvua inayoingia ndani imepitia wapi ili uzibe?. Unaweza ukawa kwenye mahusiano tu hata kwenye ndoa hujaingia siku ikatokea umemuudhi mpenzi wako ukashangaa anazira eti anasusa ana kasirika mpaka anavunja simu badala ya kumuacha na kumkimbia mshukuru Mungu kosa ulilolifanya limepelekea umejua tabia ya mpenzi wako, heri mvua ikanyesha ukajua wapi panavuja.

Jifunze kuelewa mambo kwa mlengo chanya, usiutazame sana mkono unaokuonesha mwezi ulipo ila tazama mwezi unaooneshwa. Hakuna kitu kinatesa duniani kama mtu akufanyie kitu ambacho hujui kwanini anakufanyia ama umefanyiwa, hakuna kitu kibaya kama ufukuzwe kazi halafu hujui kwanini umefukuzwa kazi, hakuna kitu kibaya kama hujui kwanini unapata hasara kwenye biashara, hakuna kitu kibaya kama Mchungaji washirika wake kuhama kanisa huku yeye hajui kwanini Washirika wanahama, vivyo hivyo kwenye mapenzi hakuna kitu kinachotesa kama ukampenda mtu sana then from nowhere akawa hakupendi tena unabaki kujiuliza maswali usiku mzima bila majibu, kuna watu wanakonda sababu ya kuwaza “why this happening to me”? kuna rafiki yangu alipelekwa kulazwa kabisa hospitali, kuna watu wanaombewa utadhani wanaumwa kumbe mapenzi yanatesa, mapenzi yana nguvu kuliko mauti.

Maisha ni changamoto jambo lolote unaloligundua kupitia “Coincidence” mshukuru Mungu badala ya kuanza kuanza kuchukua maamuzi sio, pengine kupitia kufukuzwa kazi ndo umegundua rafiki yako yuko tayari kujiua ili asiishi bila ajira,  BiBlia inasema “All thing(s) works for good”. Kama kupitia kitu Fulani au issue Fulani ndo umegundua kitu kingine basi mshukuru Mungu kwa kilichotokea sababu kimekuwezesha kujua kitu kingine. Kumtuhumu muhusika hata kosa utetezi kwa sababu moja ama nyingine. Heri Mvua ikanyesha ukajua wapi Panavuja ili uchukue hatua za marekebisho ama kuhama.

Tuko pamoja.

Papaa
0713 494110

Thursday, April 10, 2014

Exposed From Facebook........Mambo 7 Mwanaume atarajie Kupoteza anapoingia kwenye Mahusiano ama Ndoa


Marafiki Zangu Wanaotarajia Kuoa Wanaume hatuna Sehemu ya Kitchen Party Sie tunaendaga tu hivyo hivyo, tunaambiwa tusameheane, Tupendane na Kuheshimiana na mambo yanayofanana na hayo. Unapofikiria kuoa ama kuchumbia mtoto wa watu ama Kuwa na Serious Relationship kuna mambo mengi sana huwa yanatokea.

Zamani nilikuwa sijui kwanini Watu wengi sana baada ya kuoa hubadilika na wengine wanapoteza kile walichokuwa nacho kabla ya kuoa wengine hadi huduma zinakufa kwa sababu ya ndoa ukiacha sie wachache ambao baada ya kuoa ndio akili zinakuwa na afya zaidi na unaona mambo mengi ambayo ulidhani unajua kumbe haujui. Ndio maana juzi nilisema kwenye ndoa kuna mmoja amebahatika sasa unless uwe umebahatika utafurahia.
Kwa Wanaume Wenzangu Wote ambao Wanatarajia Kuingia Upande Huu Wajiandae Kwa Mambo 7 Kuyapoteza unapoingia katika Serious Relationship.

1. Marafiki Zako Wa Kike….Usitegemee Kabisa Ukishatangaza nia ya Kuoa utaendelea kuwa na marafiki wa jinsia ya kike kama zamani wale waliokuwa wanaku sms mara kwa mara, wale waliokuwa wanakusifia pale unapofanya vizuri watapungua, na humu Facebook kama ulikuwa unapata Comments 1000 au 6000 usitegemee tena usishangae kupata Comments 3-10 ni mabadiliko ya kawaida sana pale unapotangaza nia. Kabla ya Kutangaza Nia ukipost Picha Yako Facebook utashangaa ma Comment “You Look Wow”, “Handsome wa Ukweli”, “I Like Your Shirt”, “I Like Your Pause”. Ukitangaza Nia tu jua hata “Like” hautapata wengine watasema wanaogopa hawataeleweka vizuri na Mpenzi wako, kuna kuwa na adabu Fulani hivi lakini wengine Ukweli ni kwamba walikuwa wana matumaini sana na wewe.

Sababu nyingine pia ni Mpenzi wako ama mkeo hatakuwa na amani sana na baadhi ya marafiki zako wa Kike ulio nao, ajabu wewe mwenyewe hauna hata wazo la huyo mwanamke ila utashangaa tu unaambiwa “Sipendi Urafiki wako na Jack”. Kuna neno wanalitumia “I don’t feel Comfortable……” Ukishasikia tu hilo neno maana yake “STOP”. Ukimuuliza unamaanisha “Nisiwe Nachat “?atasema hapana “But am not Comfortable”

Wakaka Mjiandae haya ni mambo ya Kawaida Sana kwenye maisha kupoteza marafiki wa Kike ili Ubaki na Umpendae kuliko wote si ndio maana ulimchagua yeye.
2. Tegemea Kupoteza “Weekends” Zako. Ninaziita ‘zako” kwa sababu kabla ya kuwa na Relationship ama ndoa Ulikuwa na uwezo wa kujiamualia Weekend hii nalala, Weekend hii naenda movie, Weekend hii naenda Kulala kwa Prosper, Weekend hii naenda sijui Wapi. Kati ya vitu Wanawake nadhani karibu wote wanapenda ni kuwa na muda wa kutosha na Mpenzi wake. Tena sio uwepo tu mwili akili hazipo hapana,wengine wanatamani mtoke wote muende out na ukifika out sio uwe busy na simu yako haumpi nafasi, kumpa nafasi sio kukaa pembeni yake la hasha ni Ku-communicate. Wapenzi wengi sana Wanazungumza lakini hawa-communicate. Mwanamke anapokuwa na wewe anataka uache kila kitu kisha macho, masikio, na ufahamu uwe hapo, sio yeye anakuongelewa halafu wewe unajifanya Busy eti na Mpira. By the way hawako interested sana na story zinazokuhusu wewe anataka kusikia mambo yanayowahusu ‘nyie”. Wanawake wanamaswali ambayo wanaume wengi sana hatuna majibu unaweza shangaa uko ofisini na mpenzi wako anajua kabisa uko ofisini, ghafla unashangaa “sms” unaulizwa ‘Uko Wapi”? sasa wewe kwa kutokujua “Communication” unakurupuka tu kujibu “siii niko ofisini” hivi unadhani kwa akili zako za kawaida hajui uko ofisini??au unapoulizwa za Siku yako??jibu lake sio “Safi”, Sio “Poa”…….Jibu lazima liwe na attachments za kutosha. Wanawake huwa wanahitaji Muda na Wapenzi wao, sasa wewe usijifanye, “tunafatana fatana kama Kumbikumbi” yaani wao kufatana fatana ndo wanapenda na wao huwa wanashangaa sasa kama hutaki tufatane fatane kwanini unanioa?Usishangae kabisa Jumanne unaulizwa “Weekend Una ratiba gani”?sasa wewe badala ya ku-communicate, Una ropoka “Jamani leo Jumanne unauliza Jumamosi”?hahaha maana yake hapo “weekend ninakuhitaji”.

3. Kuchat Chat na Wadada, Kuwa na Muda na shughuli Zako Vinapotea. Sisi wanaume ni watu ambao kuna vitu wanawake huwa hawawezi kabisa kutuelewa hasa tunapokuwa kwenye mahusiano. Wanawake huwa wanashangaa sana Unawezaje kuwa na namba ya X wako. Wakati wao wakipata mpenzi mpya huwa wana delete hapo hapo. Ingawa zoezi hili lina madhara yake lakini ukweli ni kwamba wanaume wengi sana hupenda kuchat chat na wanawake. Ndoa nyingi sana zimekuwa na maugomvi pale mwanamke anaposhika simu ya mumewe amechat na wanawake kibao, au anakwenda facebook anashangaa mumewe ana marafiki wengi wa kike, mke anaenda kulala anashangaa mumewe ama mpenzi wake yuko busy na simu. Kuna wanaume ukweli ni kwamba wanapenda sana ku-Flirt yaani anaweza akawa anachat na mwanamke mambo ya mapenzi wakati hana hata wazo na huyo mwanamke. Nimekutana na issue nyingi sana za hivyo unaweza shangaa mpenzi wako anachat chat na mfua nguo wa nyumbani kwake ndio maana sio ajabu katika nyumba za kupanga za watu wengi wanaume ndio wanaokuwa na namba nyingi za wapangaji wa kike kuliko wanawake kuwa na za wanaume. Ukishakuwa kwenye mahusiano haya mambo sahau kabisa na kwa kadri unavyotaka kuchat chat mwanamke mwingine ndivyo ambavyo unaibua maswali kwa mpenzi wako wa kike utaulizwa tu swali ina maana huwezi pitisha siku bila kuwasiliana na “Chihiyo”??ili kuponya mahusiano yako basi huna budi kuwaepuka wengine na kuambatana nae huyo siku zote.


4. Kuwajibika Kwa Mpenzi Wako---Utii Pasipo shuruti…Ukiwa Single unaweza jiamulia mambo yako, unaweza jiamulia muda wa kurudi, unaweza jiamulia nini Uvae na nini Ule, wapi uende. Ukishakuwa kwenye mahusiano serious na pengine ukishakuwa umeoa ujue haupo huru tena ulishauza uhuru wako. Ukishakuwa kwenye mahusiano Mpenzi wako anatamani yeye kuwa wa kwanza kujua habari zako kuliko mtu mwingine yeyote. Kwenye saikolojia ya Wanawake wanaamini kwa kadri wanavyokuwa wa kwanza kujua habari zako hasa mpya ndivyo ambavyo wanakuwa wameshibwa kimapenzi. Hakuna kitu kibaya unasafiri kwenda Mwanza eti Mpenzi wako anaona facebook “Mwanza Moja”, ama umemwambia naenda Posta Mara moja kumbe ukapata appointment ukapita Mlimani City, ghafla mdogo wake kakuona Mcity akamtext dadake, "namuona shem amenenepa mbaya, hongera dada" nae anauliza “mmh umemuona wapi”?Yuko hapa Mcity anaongea na mdada mmoja hivi, ujue hadi hapo umenunua kesi, umeaga unaenda Posta, Kumbe umeenda Mcity kuonana na wanawake zako. Ukweli ni kwamba Yule mwanamke alikuwa anakupa deal la “Chomoza” ambalo ni faida yenu na mkeo lakini ujue hata utoe maelezo yepi kuna kitu hata kuelewa. Ulipokuwa Single ulikuwa hauwajibiki mahali ukishakuwa na mahusiano jua unawajibika kwa Mpenzi wako, anaweza asikuambie lakini ukweli ni kwamba anatamani Kuwa wa Kwanza kufahamu vitu vyako pengine kuliko Mama yako Mzazi. Hakuna kitu Kibaya Mpenzi wako wa kike anasikia kutoka kwa ndugu zako kuwa mmenunua kiwanja,anasikia kwa marafiki zako kuwa kumbe ulichukua mkopo bank. Sio kwamba wanatamani kujua ili Wakuzuie kufanya unachotaka kufanya lakini ukweli ni kwamba Wanatamani sana Wao kuwa sehemu ya moyo wako. Utalazimika kusema Yote kuliko mengine ukajifanya una ujasiri wa kumwambia ndugu zako kuliko yeye.


5. Uhuru Wako Wa Fedha Unapotea…Kati ya maeneo ambayo yameleta mzozo kwenye mahusiano ya watu wengi sana basi ni eneo la Mtonyo. Fedha zozote ambazo unakuwa nazo kabla ya Kuoa ni Zako siku ukioa hata account ikiwa na Milioni 10 ujue ni zenu. Kwa kuanza tu siku ya harusi zawadi za hela zinazotolewa sio zako mwanaume ni “zenu”. Mkeo anao Uhalali na uhuru wa kukuuliza kuhusu matumizi Yenu. Mkeo anao Uhalali wa Kuuliza Vyanzo Vyako Vyote Vya Fedha ulivyonavyo nawe kumwambia pasipo kumumunya maneno. Kama mtu anakupa mwili wake itakuwa makaratasi yako?Mwanaume ndiye Mtekelezaji wa majuku YOTE ya Nyumbani Unless itokee Mkeo atake kukusaidia, hata akiwa ana hela na unajua ana hela Mwanaume Ndiye anayewajibika KUTIMIZA mahitaji ya home pasipo mwambia “wewe hela sii unazo” Sio wajibu wake labda muwe mmekubaliana maana yeye ni Msaidizi, anasaidia pale ambapo umekwama. Hauna uhuru wa Kumkopesha mtu fedha pasipo idhini ya mpenzi wako wa kike. Hauna idhini ya kununua kiwanja ama kitu pasipo “kushauriana”. Kwa wale ambao wamebahatika Wanajua Mshahara wa Waume zao na Salary Slip wao ndio wanaozitunza, kwa wale wenzangu na mimi kazi zote za nje kuanzia u-Mc wife ndiye anayepokea advance kama mweka hazina na kuiweka anakojua yeye. Hakuna kitu kitamu kama Mpenzi wako ukampa fedha tu siku ukaamua yaani leo kazi zangu ya U-mc mwezi wa April hela yake yoote yako. Mwaka una miezi 12 kuna hasara gani Mpenzi wako akala fedha ya kazi za mikono yako za mwezi mmoja?


6. Your Identity Hupotea---Ukishaingia Kwenye mahusiano ujue sio tena wewe ila ni “nyie”. Kuna mambo ambayo umezoelea kuyafanya ukiwa Single ukishakuwa na mahusiano au mke ujue vinapotea. Muulize John Lissu ambaye alizoea kuwa shaghala maghala, lakini Wanawake wengi sana wanapenda Utaratibu hasa wa nyumba zao. Anataka kila kitu kiwe na “SPACE” anataka aweke maua yaonekane, aweke vikombe vionekane. Kabla ya kuoa nilikuwa napoteza muda mwingi sana kutafuta vitu vidogo vidogo kama Soksi, Sindano, Kiwi. Ukishakuwa na mahusiano suala la ‘wewe” linakufa na Umimi lazima ufe. Inawezekana umezoea Kulala bila kukoga, inawezekana wewe umezoea kurudia suruali na nguzo zingine hata mara 3 halafu unaona pouwa tu, mwingine amezoea kuingia na viatu mpaka chumbani. Kuna wanawake wengine unavulia viatu mlangoni ndani kuna ndala za kuvaa ndani sasa wewe mtoto pori kama mie unataka kujifanya “ndo nilivyozoea”, mwenzako amesafisha nyumba wewe unakuja na mabuti yako yenye matope kisa na mkasa wewe baba mwenye nyumba. Ukishakuwa na mahusiano Serious anza kujiandaa kupoteza vitu vingi sana ulivyozoea. Wanawake wanapenda waume zao wawe smart waonekane nadhifu.

7. UBINAFSI lazima Ufe….Kati ya mambo ambayo nadhani wanaume wengi sana wanatakiwa kuanza kujifiunza tangu utotoni ni uwezo wa kuwaza kuhusu feelings za wengine hasa jinsia ya kike. Pia uwezo wa kutoa fedha, muda pasipo kuwa na risala ndefu utadhani shirika la Mikopo. Unaweza kuta mnaenda kwenye sherehe mwanaume amepiga pamba ma bring bring ya kufa mtu sasa tazama mke wake amepiga gauni la Karume na Cheni za pale mwenge. Kila Saa unawaza “Mimi”, ama “Kwetu”, unakuta mwanaume anasimu kali Screen touch sasa katazame ya Mkewe kisa na mkasa “hawezi tumia” kwanini usimfundishe??Unaweza kuta mwanaume mwengine anatuma hela kwa mama yake wakati mkewe akitaka kuomba mpaka atume na maelezo, Jana sii nimekupa Laki 2 nipe “mchanganuo”. Kati ya Vitu ambavyo utarajie kuvizika ukiwa na Relationship basi ni “u-mimi”. Kunyamaziwa haimaanishi ndo uko sawa ila ujue “unavumiliwa”, Mpenzi wako akitaka kununua kitu mpaka aombe ila wewe ukitaka unaenda tu kutungua unayoitaka. Wewe ukijinunulia Vocha unaweka Buku 10 mpenzio akitaka Vocha unampunguzia BUKU. Wengine wakija kwa mbele za watu wanaweza toa ahadi kubwa kubwa mpaka wapenzi wao wanapatwa na butwaa “heee kumbe ana hela’?wengi wetu ni wabinafsi kupita maelezo mwingine mpaka kwenye kula unaweza kuta mume anawahi minofu minofu, sasa mko wawili tu unawahi minofu ili hizo zingine ale nani?unaweza kuta mwingine mmeenda out mpenzi wake akiagiza chakula anachotaka anaenda kusoma “bei” furaha yake kiwe na bei rahisi kuliko chake, cha mpenzi wake kikiwa na bei kuna kaukakasi kanamuingia utadhani ilipitishwa kwenye Rasimu ya Katiba Kuwa yeye ndo ale bei kubwa. Ukianza mahusiano jua tu Ubinafsi hauna nafasi.Nikirudi Tena nakuja Kuandika……..Tabia 10 za Wanawake Ma-Single Zinazosababisha Kuchelewa Kuolewa (msijipe moyo wakati wa Bwana haujafika) Kuna mambo huwa mnabugi mbayaaa matokeo yake mnapotezewa mbaya. Unashangaa una qualities zote za Kiroho, Kifedha, Kielimu na Ufahamu still watu wanakuja wanakaa kidogo kisha haooooooooo.

Tuesday, April 8, 2014

Kanisa la Magomeni TAG laadhimisha Miaka 75 ya Kanisa la TAG kwa Kualika Washirika Wote Wa Zamani

siku ya Jumapili katika Kanisa la Magomeni TAG katika kusheherekea miaka 75 ya Kuanzishwa kanisa la TAG hapa Tanzania, iliandaliwa ibada ya Kihistoria kwa Mchungaji wa Kanisa hili Dastan Kanemba Kuandaa Ibada kwa kualika washirika wa Magomeni waliowahi kusali mahali hapo na kuwa na chakula cha pamoja.

Katika ibada hiyo ziliimbwa nyimbo za mwaka 47 wakati kanisa linaanza, watoto wa Sunday School ambao kwa sasa ni watu wazima walikumbushia enzi za utoto wao kisha aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa hilo ambaye ndiye mwasisi Mchungaji Sasali alihubiri siku hiyo. Kisha chakula cha pamoja kiliandaliwa.

Akihubiri katika Ibada hiyo Mchungaji Sasali alisema Kanisa la TAG halitaweza kuvuna mavuno mengi iwapo kuna chuki kati ya mtu na mtu, kati ya kanisa na Kanisa, Yesu alipokufa alifanya kazi ya kuvunja "viambaza". Aliwataka washirika wa Kanisa hilo kuvunja viambaza vyote ambavyo yamkini watu bado wanavyo mioyoni ili kuweza kupiga hatua.
Sehemu Ya Umati Wa Waumini Waliokuwepo Kwenye Ibada
Ma Mc wa Event Ze Blogger Kushoto na Joseph Mwakibuti
Aliyekuwa Mchungaji Kiongozi wa Magomeni TAG pamoja na Mke wake Pastor Sasali akienda sawa katika Ibada hiyo
Pastor Matthew Sasali ambaye ni Mtoto wa Pili wa Mchungaji Sasali akifatilia Ibada kwa Umakini Mkubwa
Hapa Sijui Ilikuwa nini?
Mchungaji Kiongozi Wa Magomeni TAG Dastan Kanemba akitoa maelekezo Muhimu wakati wa Ibada
Ze Blogger akimpa Kisa Cha Zamani Sana Wakati Wa Kanisa hilo linaanza
Watu hawana Mbavu Ma-Mc wakiwa Kazini
Pastor Matthew Sasali akikumbushia Kinanda Enzi za Magomeni
Joel Sasali Uche wa Bongo akikamua Worship Siku ya Jumapili
Kitu Cha Cord...na Pastor Mathew Sasali
In His Presence
Ze Blogger akituma Vocal Wimbo wa Kuabudu
In His Presence...There is the Fullness Of Joy
Kitu Cha Sebene
Mtakatifu Mtakatifu Twakuita Mtakatifu Eeenh Yesu Wewe Mtakatifuuuu
Mchungaji Kiongozi wa Magomeni TAG Mch. Kanemba na Mke wake.
Mchungaji Sasali aliposimama kwenye madhabahu alipanda mama mmoja kupangusa kwa kitambaa chake miguu ya Mtumishi huyo
Mchungaji Sasa alikuwa na Mke wake Madhabahuni
Watoto wa Mchungaji Sasali

Mzee Mzima Pastor Sasali akihudumu siku ya Jumapili kwenye Ibada ya maadhimisho ya Miaka 75 ya TAG ngazi ya Kanisa la Mahali Pamoja
Pastor Sasali na Mama Sasali Wakiwaombe Watumishi Mch. Kanemba na Mke wake
Pastor Sasali na Pastor Kanemba wakifanya maombezi ya Washirika
Kwaya ya Mwaka 47 akiimba Katika Ibada, Hawa ndio waliokuwa Washirika Wa Mwanzoni Mwanzoni wakati Kanisa Linaanza
Vijana Waliofungishwa ndoa na Mchungaji Sasali wakitoa Sadaka Ya Shukrani


Papaa On Tuesday......Ganda La Muwa La Jana Chungu Kaona Kivuno

Baada ya Mapumziko ya Kukumbuka mmoja wa Waasisi wa Taifa Letu Mhe. Karume siku ya jana nimatumaini yangu ya kuwa tu wazima na tunaendelea vema na shughuli zetu za kila siku za kujiendeleza sisi wenyewe na Taifa letu kwa ujumla. 

Ikiwa na ni Jumanne yetu ya kwanza katika robo ya pili ya mwaka 2014. Maana miezi mitatu ishakatika tumeanza robo ya pili chekecha ubongo mapema.Siku ya leo nimeona ni vema tukakumbushana Papaa On Tuesday hii niliyoandika miaka miwili iliyopita kuhusu  mambo yanayoweza kutupa fursa ya kuweza kusonga mbele katika mwaka 2014. Leo kwenye Papaa On Tuesday (POT) nimeandika msemo wa Kiswahili ambao kwa wengine inaweza kupata utata wa matuzimi ya lugha yetu tukufu ya Kiswahili.

Msemo wa Kiswahili uliotumika una maana ya kwamba, ganda la muwa ambalo kwa kawaida halina matumizi tena ya kawaida kwa mwanadamu na ambalo limeshaanza kukauka, basi mdudu chungu ambaye anakula maganda hayo kwake hugeuka kuwa sherehe kubwa sana sababu ndo chakula chake, sababu hiyo ganda la muwa la jana kwa chungu kwake ni mavuno ambayo yanamsahaulisha kabisa kuwa muwa watu hawali kila siku. Lazima tutajiuliza msemo huu maana yake ni nini?

Watu wengi wanatabia ya kama ya huyu mdudu chungu. Mtu asiyezoea kuwa na kitu siku akipata hata kitu kama ni duni au hafifu ama dhaifu au hata kama ni kidogo, hushangilia na kukimaliza chote ama kukitumia chote kikaisha akisahau kuwa kesho maisha yanaendelea. Ndio maana katika kizazi chetu unakuta mtu kila mwezi ana madeni kila siku anadaiwa yeye na kuna wakati hata yeye mwenyewe anayedaiwa sio kwamba hata yeye mwenyewe anapenda ila anajikuta tu yuko mule mule ni kwamba amefungwa kwenye maisha fulani amejikuta anapiga mark time. Anadhani akipata laki moja shida itaisha anagaundua akipata laki moja pia haimtoshi

siku moja tukiwa kwenye program ya “Intellectuals Meeting” rafiki yangu na Boss wangu Eng. Andrew Mnzava alikuwa anafundisha akauliza swali “Kama leo ukisimamishwa kazi kwa muda gani utaweza kuishi maisha yale yale uliyokuwa unaishi?je miezi miwili, mitatu?”. Wengi wetu tunaishi hivi tulivyo kutokana na vipato vyetu vya sasa na vyanzo vyetu vya fedha vilivyopo umewahi kuwaza hivi siku vyanzo vyote vikisimama kuleta fedha kwa muda wa mwezi mmoja nitaweza kuishi mjini?We unadhani kwanini Wastaafu huwa wanakufa haraka mara baada ya kustaafu?hawa watu walizoea mifumo ya fedha wakiwa maofisini ambapo wakistaafu hiyo mifumo inakuwa haileti tena fedha kwao.
Si kweli kwamba watu huwa hawapati fedha katika maisha yao kila siku watu wanaingiza fedha lakini tumekuwa kama Chungu aliyepata fundo la muwa wa jana. Mtu anapata hela na alikuwa amepanga kabisa kununua kitu Fulani cha maana katika kuleta maendeleo katika maisha yako ajabu mtu anapata fedha anaenda kununua kitu kingine kabisa. Kuna watu fedha zao zinaishia kwenye kuvaa, kula na kujipodoa na katika mambo ya kifahari yasiyo na sababu eti aonekane mambo safi, huku ni kufurahia ganda la muwa la jana, masikini akipata “makalio” hulia mbwata, kwanini unapenda uonekane vile ambavyo sivyo ulivyo?

Wengi wetu tunatosheka na afadhari kwenye maisha hatupendi kwenda extra mile, unahangaika kutafuta fedha pengine kwa mshahara ama biashara mwishi wa siku hakuna jambo la maendeleo unalolifanya unajisikia raha ukionekana smart, unanukia na nadhifu wakati vyanzo vyako vya fedha vikisimama kwa mwezi mmoja wengi watageuka kuwa majambazi, Malaya na hata matapeli.

Tujijengee tabia ya kujiwekea akiba katika kile kidogo tunachopata, tujifunze kufanya ujasiriamali, tujifunze kufanya biashara, usipende watu wakufanyie kila kitu, kuwalalamikia watu kuwa hawakusaidii katika maisha haitatatua tatizo ulilonalo, kazi haitafutwi kwa kulala na kulalamika, mafanikio hayaji tu kwa kuomba na kuombewa, unao waona leo wana maendeleo kuna siku walijinyima kwa ajili ya maendeleo yao waliwahi fanya opportunity cost , wakaamua kuacha kununua Prado wakanunua Colona ili waanzishe duka, walijinyima kuvaa kwa ufahari ili wajenge flemu za maduka, wewe unataka usaidiwe huku ukiwa unaangalia TV nyumbani kwako, mtu mwingine aungue jua kwa ajili yako.

Huu mwaka unapoendelea jipange sawa sawa, kila fedha inayopita mikononi mwako weka akiba, akiba haiozi, anza na biashara ndogo mahali Mungu ataiona na kuikuza, achana na akili za masikini “tumia fedha ili ikuzoee” fedha huwa haima tabia ya kuzoea watu, ukifanyika mtumwa wa fedha unaanza kuwa mwendawazimu wa fedha hizo, jichunguze sana unafanya nini na fedha inayokuja mikononi mwako. Anza kuwazaa kufanya kitu usitosheke kuwa mama wa nyumbani ama baba wa nyumbani, siku utakayochoka utaichukia hata TV yako unayoipenda sana, siku ukichoka na maisha uliyonayo ndipo utakapoanza kupiga hatua kwenye maisha yako.

Ganda la Muwa wa jana usikufanye usikie utamu mpaka kesho na kusahau maisha yanaendelea kuwa makini na kila unachofanya ili uweze kuvuka katika maisha haya.Usitosheke na afadhari komaa na maisha kila iitwapo leo.

Think Differently Make a Difference.
Papaa
0713 494110.

Wednesday, April 2, 2014

Kila Jambo na Majira YakeKatika Kitabu Changu Cha Pili kinachozungumzia Kuhusiana na Character/ Tabia Pamoja na Mambo Ya Umaarufu. (A Gift Can Take You Up There, But Character Will Keep You Up There" niliwahi kuongea kwa muhtasari hiyo. Kati ya vitu nilivyoandika kwenye Kitabu ni Mfano wa Biblia Wa Mwanapunda aliyepandwa na Yesu.

Kwa wale waliosoma story hii maarufu ya Yesu kwenda Jerusalem alitaka Usafiri wa Kumfikisha huko anakotaka kwenda, Ukisoma ile story nimeandika mambo kama manne hivi.

1. Yesu alitaka Mwanapunda ambaye hajapandwa bado. Kama gari Yesu alikuwa anataka gari Brand New. Yesu alikuwa anataka kutumia "Unknown Punda" alikuwa anataka kumpanda "Unpopular Punda". Yesu alimtafuta Punda ambaye sio maarufu, Punda ambaye alikuwa hajulikani kabisa. Watu maarufu sana wengi wanasahau kuna wakati waliwahi kutokuwa maarufu, Walikuwa hawajulikana, na kabla ya wao kuwepo walikuwepo wengine kabla yao. Ukweli ni Kwamba walikuwepo Punda wengi sana kabla ya Punda aliyepandwa na Yesu.

2. Punda hakuwa anajua amembeba nani, Pengine Punda alipoona Watu Wanamshangilia kwa mitende na nyimbo alidhani wanamshangilia yeye pengine aliongeza na madoido mengi kwenye kutembea akidhani watu wanampenda sanaaa. Ukweli ni Kwamba watu hawakuwa wanampenda Punda isipokuwa aliyembeba. Kwani ulisoma wapi Punda aliporudi walimshangilia na kumtandikia tena. Season Yake Imekwisha tayari. Kazi yake imekwisha tayari. Watu wengi maarufu huwa wanasahau kuwa hawajawa maarufu kwa sababu ya wao wenyewe isipokuwa wamekuwa maarufu kwa sababu ya Walichobeba ndani yao. Kama wewe iko Mkristo jua hujawa maarufu kwa sababu uliamua kuwa maarufu ila Mungu alikuchagua kati ya (Punda) wengi ubebe kile ulichobeba. Watu wanapokushangilia watu wanapokupongeza usidhani wanakushangilia wewe hasa ila kile ulichonacho kile ulichokibeba. Jua kwamba kabla ya wewe pia walikuwepo watu wanafanya kitu kama hicho ama wewe umekuja kivingine. Ukiota mapembe na kiburi kumbuka watu hawakupendi wewe kama wewe ila wanapenda kile ulichobeba ndani yako. Kile ulichobeba kikiondoka ujue hakuna makofi tena kwako.

3. Umaarufu ni Season. Kati ya vitu ambavyo watu wengi wanasahau kwenye maisha ni kwamba umaarufu ni Season. Season ikiisha ujue nawewe hakuna tena. Punda season yake ilikuwa ni kubeba Yesu na Kumfikisha Jerusalem wakati huo nakuambia hata Punda angevunjika mguu watu wangembeba Punda, Punda angetaka rambaramba angepewa, hata Punda angesema hataki kanyaga Mitende anataka kanyaga Miti ya Krismas wangechuma sasa ngoja baada ya Kufika Yerusalem uone kurudi kwao Punda kama kuna mtu alimfatilia tena. Ni kweli punda ni yule yule aliyekuwa amembeba Yesu alishangiliwa na nyimbo juu kurudi hakuna mtu mwenye taarifa nae sababu gani Season imekwisha, na aliyekuwa amebebwa ameshuka. Jua leo ni season yako, Jua leo hata ukisema hauimbi bila milioni 2 watu watatoa, Ukisema hautengenezi Video bila Milioni moja watu watatoa lakini Jua kitu Seasonal Mwanangu. Kesho utasahaulika. Leo hii nani anawajua Ngurumo, Leo hii nani anamjua Waziri Sonyo, Leo nani anamjua Muhina Panduka Toto Tundu, Leo nani anamjua Bongoman aliyesababishaga Watu kutaka Kuuana kwa ajili yake, Yuko Wapi Abeid Mziba, Yuko wapi Juma Mgunda aliyekuwa anapiga mashuti mpaka mpira unapasuka, yuko wapi Hamis Thobias gag, Gagarino.....Kuwa makini sana na Season yako. Kuna wakati unafika hata ukiwaambia watu BURE watakataa sio kwa sababu haujui kufanya ila Season ndo kwishney. Sio kwamba hakuwa Punda alikuwa Punda tena Punda aliyepandwa na Yesu tatizo Yesu alikuwa kesha shuka na Season yake imekwisha.

Nikija tena nakuja kumalizia kuandika Process alivyopatikana Punda....Yesu akasema Wakiwauliza Mwambieni "Bwana anahaja Nae".....Nitaandika Kuhusu "WITO"....Bwana akisema ana haja na wewe hakuna pa kwenda, Bwana akisema ana haja na wewe hata kama kuna "mwenyewe" atakuachilia, hata kama Umeajiriwa kwenye Kampuni kubwa siku Bwana akisema Ninahaja Nawe ujue utaondoka...Punda aliondoka kutoka alipokuwa kwenda kuitikia wito......Mambo ya Kuzingatia Wito Unaanza, Kupanda Kunafuatwa, Umaarufu wa Mwisho.....Sasa Kasheshe Unataka Umaarufu Kabla Hujaitwa......

Ntarudi....

Tupeane Nasafi Kwenye Maisha...

Kama Mwili Ulivyo na Viungo Tofauti Tofauti ila vyote vinafanya kazi kwenye Mwili Mmoja ndivyo ambavyo Binadamu hatufanani. Kila mtu ameumbiwa haiba yake wengine wao ni Visible sana wengine hawapendi hata kuonekana na watu, kuna wengine wao ni waongeaji kupita maelezo lakini kuna wengine wao ni wasikilizaji si kwamba wengine sio bora sana kuliko wewe ulivyo. Kuna wengine ingawa hawana "heshima" sana kama wale wanaoonekana lakini haimaanishi wale wasioonekana hawana heshima.

Ukienda kwenye nyumba zetu kuna sahani huwa hazitumiki au glass hazitumiki mpaka waje wageni tena wageni wale wa maana kutumika sana kwa glass haimaanishi yenyewe ndo bora sana kuliko ile inayokaa mwaka mzima kabatini. Kuna vyombo vya Sebuleni na Kuna vyombo vya Jikoni. Kwa utamaduni wetu wengi sana itakuwa ni ajabu chujio la nazi, Chujio la Chai na Mwiko Kukaa Sebuleni, ama tukachukua makochi na Kupeleka Jikoni kwa namna vilivyo dezainiwa vinapaswa kukaa kila kitu sehemu yake. Makochi Kukaa Sebuleni sio kwamba yana heshima sana kuliko Sufuria la kupikia kila mtu ana heshima yake inapofika saa yake ya kazi. Haiwezekani wageni wakaja wakakalia Sufuria ama Wakakalia Mwiko. Kwa kawaida Watakalia Makochi. Saa ya Kupika hatutumii Tv tunatumia Sufuruia, Kukaa Kwa Jiko-Jikoni haimaanishi lenyewe sio bora kuliko Flat Screen ya Sebuleni.

Kuna watu wanaonekana kama hawana heshima kwa sababu tu hawaonekani kama wengine. Matokeo yake wale ambao Mungu aliwaumba wasiwe watu watu wa kuonekana Wanapotaka Kuonekana wanafanyika Kituko Cha dunia. Ukiwa Mzuri sana ama Mrefu sana ama wa namna gani haimaanishi lazima uonekane kama wengine wanavyoonekana. Hata Ukiwa na sehemu za Siri nzuri namna gani, au pana namna gani au ndefu namna gani zimeumbiwa kuwekwa ndani ya nguo. Siku mtu akizitembeza hadharani sehemu zake nzuri za Siri uke/uume watu watamwona wa ajabu si kwa sababu sio nzuri, sio kwa sababu hazifai lakini hazijaumbiwa kukaa nje. Umuhimu wake unajulikana saa yake ikifika, hata mguu ungekuwa unahamu namna gani kuwa wenyewe ndio utumike sehemu ya haja kubwa chooni haiwezi kuwa hivyo na ikifika time ya haja kubwa hakuna mbwembwe utulivu unahitajika ukileta mbwembwe saa ya haja kubwa umeweka mzigo pembeni. Pamoja na viungo vingine kuto kuonekana masaa mengi lakini asikuambie mtu Mkojo Ukubane barabarani, hautaweza kufanya lolote mpaka uutoe kwanza, wee si unajua mkojo huwa unabana sana unapofika nyumbani hata kama unapenda TV namna gani break ya kwanza Toilet unamaliza kisha ndo unakuja kwenye TV.

Kama Mungu alikuumba Uwe wa Kuto Kuonekana Kaa Kule kule Uliko Saa itafika tu ambapo kila mtu atajua umuhimu wake ni sawa sawa na dole gumba la Mguu saa zote liko kwenye viatu ngoja sasa likatike uone Balance ya Mtu hadi mwendo unabadilika. Usitake kuonekena ili uwe kama wengine ambao wewe unadhani kwa kutokuonekana umedharauliwa Its a matter of Time Saa itafika na hivyo hivyo Ulivyo utapata heshima. Ukitaka kutafuta heshima utajikuta unachekwa na kuharibu mara kwa mara kwenye maisha sababu gani?wewe umeumbiwa tofauti na wengine.

Wale wanaoonekana ambao wengi sana wamejikuta wamekuwa maarufu wamekuwa wakiwadharau sana wasioonekana kwa sababu tu wao wamepata heshima na umaarufu. wanamuziki wanasahau kuna wapigaji waliosababisha wafike hapo kuna ma-producer waliosababisha. Siku wao wakigomea kufanya kazi na wewe itakula kwako. Ni kweli kwenye Cover Picha zao hazitoki, Ni kweli majina yao yanaandikwa kana kwamba yasionekane, hata kwenye movie majina yao yanapelekwa haraka haraka mwishoni na sifa zinabaki kwa steering. Hii yote haimaanishi Steering ni bora sana kuliko wale waliopaka make Up. Ubora ama Umuhimu wa mtu ni Wakati tu.

Inawezekana Kabisa Super Star hujajua umuhimu wa yule asiye Super Star kwa sababu "muda haujafika". Muda ukishafika ndipo unapofahamu umuhimu wa mtu. Hatuwezi kufanana wote duniani kila mtu ana umuhimu wakati wake unapofika. Usimdharau mtu leo eti kwa sababu wewe ndio muda wako wa kutumika, na wewe ambaye muda wako haujafika usijione wewe ni mnyonge na usiyefaa.

Its a Matter Of Time...

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...